Tuesday, July 19, 2011
NDUGU ZANGU HII SI PICHA YA KUPIGWA KTK VIDEO HII ILIKUWA LIVE, NI KTK MAIGIZO YA KIFO CHA CHA YESU KRISTO KTK KANISA LA CCC LILILO UPANGA JIJINI DAR
Thursday, June 30, 2011
BONGE LA MHARUSI KATI YA DADA YETU ESTER KILANGO NA MMEWE RICH
WAAAAAOOOOH!!! WATOTO WA ASKOFU B. MWAKIBORWAA WALIMSINDIKIZA DADA YAO ESTER KTK HARUSI HIYO IRINGAAAAAAAAAAAAAAAA
Tuesday, June 21, 2011
PIPOOOOOO!!! J SISTERS WAPO TAYARI KWA UZINDUZI DAR ES SALAAM
WAIMBAJI HAO TOKA KTK KANISA LA MITO YA BARAKA CHINI YA ASKOFU BRUNO MWAKIBORWA WAMEDAI WANATARAJIA KUONESHA KITU CHA TOFAUTI KTK MZIKI WA INJILI KUTOKANA NA MAZOEZI YA KUTOSHA WALIOJIANDAA NAYOO
KUNDI HILO LINAUNDWA NA KINA DADA WA NNE(4) TOKA FAMILIA YA MZEE MSHAMMA NA MAMA MSHAMA AMBAYE PIA NI MBUNGE WA JIMBO MOJA HUKO BUKOBA
KINA DADA HAO AMBAO BADO WAPO MASOMONI AMBAPO WAWILI KATI YAO WANASOMA NCHINI MAREKANI NA WAWILI WAPO HAPA HAPA
KWAKWELI TUNA VITU VINGI VIGENI TUTAVIONESHA SIKU YA UZINDUZI WETU HII NI KUTOKANA KUHUDHURIA MATAMASHA MENGI NJE YA NCHI NA KUJIONEA WANAVYOFANYA HIVYO NA SISI TUTAWAONESHA WATANZANIA SIKU HIYO KITU CHA KIPEKEE NA ZAIDI TUNAOMBA MUNGU ILI SIKU HIYO IKAWE YA TOFAUTI KTK MAISHA YA KILA MMOJA ATAKAYE KUJA KTK UZINDUZI WETU. ALISEMA MWANADADA JENIFFER.
WASANII WA BONGO MOVIE WAMTEMBELEA MH MAKALAA...
Klabu ya Michezo ya wasanii wa filamu, Bongo Movie Club leo mchana walimtembelea Mbunge wa Mvomero (CCM), Amos Makalla na kupata ‘menyu’ ya mchana pamoja
Makalla, aliwaalika wasanii hao nyumbani kwake ili wawe pamoja kabla ya mechi ya leo, itakayokutanisha Klabu ya Bongo Movie na Timu ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Bunge Sport Club).
Leo, kuanzia saa 10 alaasiri kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kutakuwa na mechi mbili, soka na netiboli.
Bongo Movies wanaume watashuka dimbani kukipiga na klabu ya soka ya bunge, wakati mastaa wa kike watapekechana na waheshimiwa wanawake katika mechi ya netiboli.
Baada ya chakula, Katibu wa Bongo Movie Club, Salum Mchoma ‘Chiki’ alisema kuwa Makalla ameonesha uungwana kwa kuwaalika kwenye chakula.
Alisema, tangu walipofika Dodoma, Makalla ndiye amekuwa mfadhili wao mkuu lakini wakadai kuwa hiyo haifanyi washindwe kuifunga Bunge leo.
Naye Makalla katika kupokea shukurani hizo, alisema Bunge limejiandaa na mechi hiyo itaisha kwa Bongo Movie kulala.
Saturday, June 18, 2011
MASKINII!!!! STAA WA ZE COMEDY APATA AJALI YA KUSIKITISHAAA

Wasanii wenzake na Bambo wakiwa na sura za majonzi mara walipofika hospitalini kumwona mwenzao Dickson Samson Makwaya a.k.a Bambo aliyelazwa kitandani. Picha inayofuata ni dereva wa pikipiki waliyopata nayo ajali alfajiri ya leo.Mkali wa maigizo ya kuchekesha Bongo, Dickson Samson Makwaya a.k.a Bambo alfajiri ya leo amepata ajali mbaya ya pikipiki na kuvunjika mguu wake wa kulia sehemu ya paja.
Ajali hiyo imetokea eneo la njia panda Kigogo jijini Dar es Salaam ambapo gari aina ya DCM iliigonga pikipiki aliyokodi Bambo wakati akirudi nyumbani kweke. Dereva wa pikipiki aitwae Jumbe Juma kwa sasa hali yake ni mbaya na wote wamelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
Bambo aliyejitwalia umaarufu mkubwa miaka ya 90 akiwa na Kundi la Sanaa la Kaole ambalo lilikuwa likirusha maigizo yake kupitia runinga ya Independent Television ‘ITV’ kwa sasa alikuwa chini ya kundi la Ze Comedy ambalo hurusha michezo yake kupitia runinga ya East Africa Television (EATV).



