Klabu ya Michezo ya wasanii wa filamu, Bongo Movie Club leo mchana walimtembelea Mbunge wa Mvomero (CCM), Amos Makalla na kupata ‘menyu’ ya mchana pamoja
Makalla, aliwaalika wasanii hao nyumbani kwake ili wawe pamoja kabla ya mechi ya leo, itakayokutanisha Klabu ya Bongo Movie na Timu ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Bunge Sport Club).
Leo, kuanzia saa 10 alaasiri kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kutakuwa na mechi mbili, soka na netiboli.
Bongo Movies wanaume watashuka dimbani kukipiga na klabu ya soka ya bunge, wakati mastaa wa kike watapekechana na waheshimiwa wanawake katika mechi ya netiboli.
Baada ya chakula, Katibu wa Bongo Movie Club, Salum Mchoma ‘Chiki’ alisema kuwa Makalla ameonesha uungwana kwa kuwaalika kwenye chakula.
Alisema, tangu walipofika Dodoma, Makalla ndiye amekuwa mfadhili wao mkuu lakini wakadai kuwa hiyo haifanyi washindwe kuifunga Bunge leo.
Naye Makalla katika kupokea shukurani hizo, alisema Bunge limejiandaa na mechi hiyo itaisha kwa Bongo Movie kulala.
No comments:
Post a Comment