Saturday, May 28, 2011

MASKINI LINAH NA AMINI VULULU VULULU...



Uhusiano wa kimalavidavi uliovuma sana kwenye vyombo vya habari wa wasanii toka THT,Linah na Amini umefikia kigoma mwisho wa reli baada ya kila mmoja kufunguka kuwa wamemwagana...!

AMINI MWINYIMKUU na LINAH SANGA WOTE NI BONGO FLAVA ARTIST, WALIFUNGUKA NA KUSEMA,

Linah alifunguka “Tulikaa tukakubaliana na kila mmoja akaridhia kuwa iwe mwisho wa uhusiano wetu hivyo sababu siwezi kuweka wazi ila mashabiki wangu wajue tumeachana,”...Huku Amini nae alisema....“Dah! bwana ndiyo hivyo kila mtu kwa sasa yupo kivyake ila uelewe sipendi kuzungumzia uhusiano wetu sababu haunisaidii chochote katika muziki wangu.” Inasemekana kuwa wimbo aliouimba Linah wa Bora Nikimbie ulikua ni kutoka moyoni coz inadaiwana Amini alikuwa na tabia ya kumpa kipigo Linah mara kwa mara kitendo ambacho alikuwa anakivumilia na kufikia hatua ya kumwagana!

" Kwa kweli walipotoa tu nyimbo zao zijulikanazo kama Bora nikimbie wa Linah na Ndiyo unikimbie wa Amini, watu walishajua kabisa kwamba hawa wasanii wamemwagana na sasa kila mmoja anatafuta jinsi ya kutoa machungu yake baada ya kuachana".

1 comment:

Anonymous said...

kp updating your status meeen......n put more new comedy scene!!!@masanja mkanda naniiiiii