Saturday, June 18, 2011

MASKINII!!!! STAA WA ZE COMEDY APATA AJALI YA KUSIKITISHAAA


Wasanii wenzake na Bambo wakiwa na sura za majonzi mara walipofika hospitalini kumwona mwenzao Dickson Samson Makwaya a.k.a Bambo aliyelazwa kitandani. Picha inayofuata ni dereva wa pikipiki waliyopata nayo ajali alfajiri ya leo.

Mkali wa maigizo ya kuchekesha Bongo, Dickson Samson Makwaya a.k.a Bambo alfajiri ya leo amepata ajali mbaya ya pikipiki na kuvunjika mguu wake wa kulia sehemu ya paja.


Ajali hiyo imetokea eneo la njia panda Kigogo jijini Dar es Salaam ambapo gari aina ya DCM iliigonga pikipiki aliyokodi Bambo wakati akirudi nyumbani kweke. Dereva wa pikipiki aitwae Jumbe Juma kwa sasa hali yake ni mbaya na wote wamelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.


Bambo aliyejitwalia umaarufu mkubwa miaka ya 90 akiwa na Kundi la Sanaa la Kaole ambalo lilikuwa likirusha maigizo yake kupitia runinga ya Independent Television ‘ITV’ kwa sasa alikuwa chini ya kundi la Ze Comedy ambalo hurusha michezo yake kupitia runinga ya East Africa Television (EATV).

2 comments:

Anonymous said...

POLE SANA KAKA BAMBO!!NAIMANI MUNGU YU PAMOJA NAWE!!
NASI TWAKUOMBEA UPONE HARAKA URUDI KAZINI KAKA JAMIII INAKUHITAJI!!
WABO

Anonymous said...

getwelll bambooo!!!!!!!